Katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja 2024, Gold Micro Credit and Insurance Agent Company Limited walijitokeza kushiriki kwa dhati kwa kurudisha kwa jamii kwa kushirikiana na kituo cha Bright Light organization kilichopo Geita mjini (mseto).Hafla hii ilifanyika tarehe 07/10/2024, ililenga kutoa msaada na hamasa kwa watoto wanaoishi katika kituo hicho, ambao ni sehemu ya jamii yenye uhitaji mkubwa wa msaada wa hali na mali.
Katika hotuba yake mkurugenzi wa Gold Micro Credit and Insurance Agent Co LTD alisema "Tunatambua kuwa wateja wetu ni kiini cha biashara yetu, na katika wiki hii maalum ya kuadhimisha huduma kwa wateja, tumeona ni vyema kurudisha shukrani kwa jamii kwa kuchangia kule ambako msaada unahitajika zaidi.Hii ni sehemu ya dhamira yetu ya kuwahudumia si tu wateja wetu, bali pia jamii kwa ujumla, aidha aliwaasa watoto kusoma kwa bidii na kuwa na nidhamu.
Watoto wa kituo cha Bright Light walipokea msaada huo kwa furaha wakiwa na tabasamu walitoa shukranui zao kwa maneno ya upendo na sala. Mkurugenzi wa kituo hicho Bw Mathew alitoa hotuba ya shukrani akisistiza umuhimu wa msaada huo kwa watoto.
Kwa ujumla shughuli hii imeacha alama ya kudumu kwa watoto wa kituo cha Bright Light Organization na imethibitisha dhamira ya Gold Micro Credit and Insurance Agent katika kuboresha maisha ya jamii wanayoihudumia.